MAKOSA 10 HATARISHI YA MATUTIMIZI YA KONDOMU

Makosa 10 Hatarishi ya Matumizi mabaya ya Kondom Usiyoyatilia mkazo

1. Kutoangalia kama imeharibika

Watu wengi hutoa kondom na kuivaa pasipo kuangalia kama kuna matundu yanayo onekana kwa macho au haipo katika halia nzuri.

2. Kutokuangalia kama imeisha muda wa matumizi(expire date).

Kati ya asilimia 61 ya watumiaji wa kondom hawana muda wa kuangalia kama zimeisha muda, kutokana na ukweli kwamba hata anapopewa huificha haraka kwa kuichimbia mfukoni na kuifungua wakati wa tukio.

3. Kutojadiri na mwenza wako matumizi ya kondom kabla ya tendo.

watumiaji wengi wa kondom hawajadiri, matumizi ya kondo badala yake inakua kikwazo pale muhusika mmoja wapo atapotoa sharti la kutumia. hii itapeleka kondom kutotumika ipasavyo sababu ya kutoridhiana matumizi yake kabla. Mshiriki mmoja anaweza kufanya ujanja hata wa kuitoboa labda kwa kuhisi amelazimishwa kuitumia bila ridhaa na kutopata raha aliyohitarajia. Jadiri matumiz mazuri ya kondom kabla ya tendo na mwenza wako na mridhiane

4. Kuchelewa kuvaa kondom.

Watu wengi hupenda kujifanya wamesahau kondom na kujikuta wakitaka kuingiliana kidogo na baadae kuvaa kondom wakiamini kua ile mara ya kwanza haina madhara, jua kwamba hata muingiliano mdogo tu waweza leta madhara kama mimba na magonjwa ya ziana sababu ya maji maji ya mwanzoni yanayotoka kutokana na matamanio ya kingono.

5.Kutokuacha nafasi wakati unapo ivaa.

watu 7 kati ya 10 hawaachi nafasi wanapo vaa kondom hii inapelekea kutojua kuwa uachaji nafasi usaidia kondom isipasuke na pia shahawa zipate nafasi ya kujilundika ili zisije kutokea mwishoni mwa pindo shinani.

6. Kuvaa ndivyo sivyo

Asilimia kubwa sana ya watu huvaa kondom nje ndani au kuigeuza, hii pia ni hatari iwapo itakua ni mara ya pili baada ya tendo kupelekea kujigusisha maji ya mwanaume na kuhatarisha tendo zima kutokua salama, hakikisha unaiangalia vzr kabla ya kuivaa nakujua nje ni wapi na ndani ni wapi.

7. Kondom kupasuka

Asilimia 29 za watu huripoti kondom kupasuka, hii inatokana na kutojua kuitumia vizuri na makubariano baina ya wenza.

8. kondom kutoka wakati wa tendo

hii hutokana na kondo kutovaliwa vizri na mtumiaji kutojua aina ya kondom inayo mkaa vyema. kama unahitaji usalama wa kula vizuri lazima ujue radha ya chakula chako, jua aina ya kondom inayokutosha vyema na upo na ustadi wa kuitumia.

9.Kuwahi kutoa kondom

asilimia 13 ya wanaume wameripoti kutoa kondom mara tu wamalizapo tendo, na kupelekea wenza wao kupata mimba au maambukizi ya zinaa, malalamishi ya asilimia 11 ya wanawake kupata magonjwa na zinaa au mimba yameripotiwa wakati wenza wao wametumia kondom. hii inatoka nakujipakaza maji maji ya mwisho yanayokua yanaishia na matumiz ya kutojua ya kondom.

10. Kutovaa kabisa kondom

Aslimia kubwa sasa ya vijana kwa wazee wamekua na kujidanganya kua maambukiz makubwa ni kutokojolea kwenye uke wa mwanamke, lakinin kumbuka kitendo hichi kinamsisimko unao weza kukufanya ushindwe kumudu kutoa kwa haraka, pia kuna kutoa maji maji ya mwanzon ambayo husababishwa na muhemuko wa kingono.... baki salama tumia kondom kwa uhakika na acha michepuko
Share this article :

Post a Comment

 
Support : | |
Copyright © 2011. JAMII MIXER - All Rights Reserved
Published by S.M