Israel yajenga makaazi zaidi ya walowezi

Israel yajenga makaazi zaidi ya walowezi

Serikali ya Israel imeidhinisha ujenzi wa nyumba mpya zaidi ya 1,000 katika makaazi ya Wayahudi kwenye maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israel.
Nyumba za Wayahudi katika maeneo ya Wapalestina
Waziri wa Makaazi wa Israel, Uri Ariel, alisema nyumba hizo zitajengwa Ufukwe wa Magharibi na masahriki mwa Jerusalem ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Israel.
Tangazo hilo limetolewa siku tatu kabla ya mazungumzo ya amani baina ya Israel na Wapalestina kuanza tena mjini Jerusalem.
Waziri wa Makaazi wa Israel ametoa idhini ya mwisho kujenga karibu fleti 1,200 katika maeneo yenye makaazi ya Wayahudi, siku tatu tu kabla ya mazungumzo ya amani kati ya Israeli na Palestinian kuanza tena.
Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, alishikilia kwa muda mrefu kwamba hatarejea kwenye mazungumzo bila ya Israel kusitisha kujenga makaazi mepya kwenye maeneo inayoyakalia.
Lakini hatimaye alikubali kushiriki katika mzungumzo baada ya Israel kusema kuwa itawaachilia huru wafungwa wengi wa Kipalestina.
Makaazi ya Wayahudi katika Ufukwe wa Magharibi ndio swala kubwa linalokwamisha mazungumzo.
Makaazi hayo yanaonekana kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa, ingawa Israel inapinga hilo.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : | |
Copyright © 2011. JAMII MIXER - All Rights Reserved
Published by S.M