CUF yalaani waliomwagia tindikali wageni

CUF yalaani waliomwagia tindikali wageni

Zanzibar. Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar, kimeelezea kushtushwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Kiengereza usiku wa Agosti 7 katika maeneo ya Mji Mkongwe Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Salim Biman, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma ilisema CUF inalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia tindi wageni hao ,na kinawataka polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wa kina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Taarifa hiyo ilisema: “Matokeo haya ya kikatili ya kumwagiwa kwa watu tindikali yamekuwa yakishamiri siku hadi siku ndani ya Visiwa vya Zanzibar,ambayo yamekuwa yamewathiri watu kadhaa tena bila ya wahusika kupatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria kiasi ambacho sasa jamii ya Wazanzibar imejengeka katika hofu juu ya usalama wa maisha yao ya kila siku.”
Ilisema taarifa hiyo: “Hii ni dalili mbaya kwa Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.
CUF ilisema tukio hilo kwa wageni hao waliokuwa wakifanya kazi ya kufundisha shule za msingi kwa kujitolea ni la kusikitisha na linahujumu elimu na sekta ya utalii Zanzibar na kwamba wakati umefika kwa kila Mzanzibari kupinga.
kwa dhatimb.
iokuwa wakijitolea Zanzibar kwa kazi za usomesha katika skuli za msingi hiri kuwa Sekta muhimu inayotegemewa katika kukuza uchumi wa Zanzibar (utalii)inaweza kutetereka.”
CUF inawataka wananchi wote wa Zanzibar kutoa kila aina ya ushirikiano kuweza kufanikisha kukamatwa wahalifu hao na hatimaye kufikishwa katika sehemu husika.
‘‘Sambamba na hilo Chama cha Wananchi kinawataka wananchi wote, polisi jamii kutoa kila aina ya ushirikiano kwa polisi ili waweze kukomesha kabisa vitendo vyote vya kihalifu ndani ya nchi kwa lengo la kuiendeleza sifa ya asili ya Zanzibar isemayo kuwa Zanzibar ni njema atakae na aje’’ ilisema taarifa hiyo.

 

Share this article :

Post a Comment

 
Support : | |
Copyright © 2011. JAMII MIXER - All Rights Reserved
Published by S.M