WEMA Isaac Sepetu amefungua ukurasa mwingine, amezua mjadala wa
kimapenzi juu yake baada ya kusambaa kwa picha zake tata za kimahaba
akiwa na kidume ambaye jina lake halikupatikana.
Tukio hilo
lilichukua nafasi katika mtandao wa BBM wikiendi iliyopita ambapo mara
tu baada ya Wema kutundika picha hizo kwenye ukurasa wake bila kusema
chochote, marafiki zake walianza kuzishambulia kwa kuzitolea maoni.
Picha
hizo zilizomuonesha Wema akimbusu jamaa huyo shavuni ziligeuka gumzo
pale baadhi ya watu walipodai kuwa huenda ndiye ‘bwana’ke’ mpya baada ya
kuachana na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’.
“Wema bwana! Hebu angalia hilo busu, linaonesha hisia kabisa,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo.
“Huyu
Wema ‘anaanzaga’ hivihivi kama ilivyokuwa kwa Diamond,” ilisomeka
sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa mkono na wengi.
“Jamani
mwacheni shosti wangu, hata yeye ana hisia zake kwa sababu naye ni
binadamu,” ilisomeka sehemu nyingine iliyokuwa ikimtetea Wema.
Hata hivyo, baada ya kuona maswali yanakuwa mengi, Wema alizichomoa picha hizo na kuwaacha watu na viulizo.
Ili
kuondoa utata juu ya picha hizo, Amani lilifanya jitihada za kumpata
Wema anayetisha katika filamu za Kibongo lakini ziligonga mwamba huku
rafiki wa karibu akitonya kwamba hayupo nchini ametimkia Dubai kwa
majukumu binafsi.
Post a Comment